Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa “Wanahabari wa Ahlul-Bayt (a.s)” umefanyika leo asubuhi kwa mnasaba wa Dhul-Hijjah, kwa ushiriki wa wanahabari na wasomi kutoka Iran na Bara la Afrika, kwa juhudi za Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) Mjini Qom.
Tukio hilo limeandaliwa na Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) – ABNA – kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Karamat, kwa lengo la kuimarisha mawasiliano ya habari kati ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) duniani na kuimarisha juhudi za pamoja katika kueneza mafundisho ya Kiislamu kwa njia ya vyombo vya habari.
Katika mkutano huo, wahudhuriaji walibadilishana tajiriba kuhusu changamoto za kazi ya habari katika jamii za Waislamu, njia za kukabiliana na upotoshaji wa habari dhidi ya Uislamu, na nafasi ya wahabari katika kulinda utambulisho wa Waislamu wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s), hasa vijana katika mazingira ya mashambulizi na uvamizi wa kiutamaduni (cultural invasion).
Pia, wahabari kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika walipata fursa ya kuelezea juhudi zao za kitaaluma katika kutangaza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), pamoja na kushiriki mijadala ya kistratejia kuhusu mustakabali wa vyombo vya habari vya Kiislamu barani Afrika.
Kwa mujibu wa waandaaji, mikutano ya aina hii inalenga pia kuweka misingi ya ushirikiano wa habari, usaidizi wa kitaalamu na mabadilishano ya kitaaluma baina ya wahabari wa Ahlul-Bayt (a.s) duniani kote.
Mkutano ulifungwa kwa dua na ahadi ya kuendeleza mshikamano na ushirikiano wa habari kwa ajili ya kulinda haki, kutetea waonewa (wadhulumiwa), na kueneza nuru ya Uislamu sahihi duniani kote kwa mujibu wa Mafunzo na maelekezo sahihi ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (as) wake Watoharifu.
Karibu utizame pamoja nasi picha hizi za tukio hili tulizokuwekea hapa chini
Your Comment